Huu nd’o mkwanja wa Floyd Mayweather mezani wa ajili ya chakula tu !
Huenda watu wanamfahamu Floyd Mayweather sio
kwa sababu labda kila mtu anapenda mchezo wa Boxing.. au kila mtu
anampenda, kiukweli wako wanaomfahamu kwa sababu ya mbwembwe zake, vioja
vyake kwenye media, au labda watu wanamfahamu kwa sababu ni
mwanamichezo ambaye analipwa pesa nyingi zaidi duniani kwa sasa!
Tunaisubiri May 2 2015, kila kilichosemwa itakuwa ndio mwisho wake kuhusu nani mbabe kati ya Mayweather na Manny Pacquiao,
huku vichwa vya habari Magazetini duniani na mitandaoni vikiwa na story
nyingi sana kuhusu wao tangu siku ya kwanza jamaa walipotia saini
kwamba YES watapigana.
Nikusogezee kingine cha Floyd
mtu wangu.. taarifa kuhusu yeye kwa leo ni juu ya kiasi cha pesa
ambacho jamaa anakitoa kwa ajili ya chakula tu, yani ile diet yake mpaka
siku ambayo watakuwa ulingoni na Manny.
Dola 4,000 kwa siku ndio kiasi ambacho Floyd
atakuwa akilipa kwa siku kwa ajili ya chakula tu, na hesabu iliyofanywa
ni kwamba mpaka May 2 atakuwa ametoa Dola 184,000, kwa Bongo ni kama
Mil.330/= kwa ajili ya chakula ambacho kinaandaliwa na mpishi wake Chef Q.
Kwa hesabu zetu ni kiasi kikubwa
sana cha pesa, mwingine anaona ni kama mtaji wa biashara kubwa ambayo
anawaza labda kuifanya, lakini Chef anasema hicho ni kiasi kidogo sana cha pesa kwa uwezo wa Floyd, haimpi shida kuilipa.
Moja ya vitu ambavyo wanamichezo wanashauriwa sana kujali ni ishu ya mpangilio mzuri wa chakula, Floyd anaangalia hilo pia na sio gharama za yeye kupata huduma hiyo mtu wangu. Hutopitwa na habari yoyote inanifikia na niko tayari kukutumia kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment