Thursday, March 19, 2015

TIMU ZA ENGLAND MAJANGA TENA

Klabu Bingwa Ulaya kuna hii ya jana Man City VS Barcelona…

Barcelona-1-0-Manchester-City-d-745x483Timu ya Barcelona jana usiku ilifanikiwa kuwaondoa Manchester City katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya baada ya kufanikiwa kuwafunga bao 1-0, katika dakika ya 31, baada ya Ivan Rakitic kuitumia vema pasi nzuri kutoka kwa Lionel Messi.
Dakika za mwisho Man City walipata penati lakini Sergio Aguero akashindwa kuwapatia Man City ushindi kwenye penati hiyo.
Kufuatia matokeo hayo Man City wanakuwa wameondolewa katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-1 ambapo katika mchezo wao wa kwanza Man City walifungwa goli 2-.
Hakuna story itakayokupita , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment