Hiki alichokifanya kuutoa ujauzito wa mpenzi wake ni ishu ambayo imechukua headlines !

Jamaa huyo alifanya ukatili huo baada ya
kumuwekea mpenzi wake vidonge ya kutoa mimba kwenye kinywaji alichokuwa
anakunywa kwa lengo la kumtoa ujauzito wa miezi minne aliokuwa nao,
ambapo alifikia hatua hiyo baada ya kumshawishi kuutoa kwa muda mrefu
bila mafanikio.
Mwanamke huyo amesema mpenzi wake
alikuwa akimshawishi mara nyingi kutoa ujauzito huo lakini hakukubaliana
nae, baada ya kunywa kinyaji hicho alisikia maumivu makali ya tumbo na
ujauzito wake kutoka, alipoenda Hospitali na kufanya vipimo ilionekana
ujauzito wake umeharibika tayari.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo alikiri
kufanya kosa hilo na kusema anajisikia vibaya ila amefanya hivyo kwa
sababu ilikuwa njia pekee ya kufanikisha lengo lake kuutoa ujauzito huo,
Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka saba jela.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment