Tuesday, March 17, 2015

SITUMII DAWA NA KUONGEZA NGUVU------MANNYPACQUIAO

Kuna ukweli wowote Manny Pacquiao kutumia dawa za kuongeza nguvu?

manny4Kulikuwa na sintofahamu kuhusu uwezo wa bondia maarufu duniani Manny Pacquiao, zikawepo tetesi pia kwamba Pac anatumia dawa za kuongeza nguvu, wakati huo dunia nzima iko attention kuisubiri May 2 2015 Pac na Floyd Mayweather watakapokuwa wakipambana.
manny2
Pac ameamua kukata mzizi wa fitima kwa kuamua kufanya vipimo vya damu yake ili kudhibitisha kama kuna ukweli wowote kwenye tetesi za bondia huyo kutumia dawa hizo.
manny3
Wakati Pac akifanyiwa vipimo hivyo alikuwa akioneshwa live na Televisheni ya Ufilipino huku akiwa hana hofu yoyote.
manny1
Pambano hilo la kimataifa linasubiriwa na watu wengi duniani kote huku mabondia wote kila mmoja akiwa katika maandalizi ya nguvu kumkabili mwenzake.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia  www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment