Manchester United yamtengea Cristiano Ronaldo kitita hiki ili kumrudisha Old Trafford

Kumekuwa na uvumi kuwa mchezaji huyo
haridhishwi na maisha anayoishi katika klabu yake ya sasa ya Real Madrid
na huenda safari yake ya kurudi Manchester United ikiwa kweli baada ya
viongozi wa timu hiyo kuanza mazungunzo na bosi wake Jorge Mendes.
Kwa mujibu wa gazeti la Metro la Uingereza, United ina matumaini ya kumpata Ronaldo kwa kitita cha Euro millioni 100 ambazo ni sawa na pauni millioni 71.1.
Uhakika wa raia huyo wa Ureno kukubali kurudi Manchester United upo juu yake ,licha ya kuipenda klabu hiyo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment