Sunday, March 15, 2015

ARSENAL ILIVYOICHACHAMBUA WEST HAMU JANA

Matokeo ya Arsenal vs West Ham yasikupite, yako hapa!!

giroudArsenal ilipata ushindi mzuri dhidi ya West Ham huku ikijiandaa kwa mchuano mkali kati yake na klabu ya Monaco siku ya jumanne.
Kilabu hiyo iliyopo chini ya Wenger iliishinda West Ham kwa jumla ya mabao 3-0 na kuimarisha ndoto yake katika nafasi nne bora kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza.
The Gunner ilitawala mechi hiyo huku Olivier Giroud akifunga bao la kwanzadk45 kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
giroud2Mabao ya dakika za mwisho ya Aaron Ramsey dk 81 na Mathiew Flamini dk 84 yaliifanya Arsenal kufikisha pointi 57 zikiwa ni pointi nne mbele ya mabingwa wa zamani Manchester United walio katika nafasi ya nne.
Arsenal sasa inajianda dhidi ya Monaco ya nchini Ufaransa siku ya jummane katika mechi ya ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment