Sauti ya KAJALA, SHAMSA FORD, QUEEN DARLEEN na mtoto wa Marehemu John KOMBA

Sauti ya Shamsa Ford na Kajala waigizaji wa Bongo Movie, Queen Darleen
 msanii wa Bongo Fleva wamesikika kwenye  project yao ya wimbo wa kupambana na mauaji ya albino TZ.
Shamsa amesema manager wake alimfikishia taarifa za idea hiyo naye akakubaliana nayo.
Kajala amesema alipewa taarifa na manager wake, wakakubaliana kuungana na wasanii wengine wa kike ili kuufanya wimbo huo.
Queen Darleen
 amesema anaamini kuungana huko ni kitu endelevu kwa kuwa wanawake ni 
walezi wa familia ambao mambo mengi yanakuwa yanawahusu moja kwa moja.
Mtoto wa Marehemu Kapteni John Komba, Herman John Komba
 ambaye amesema siku nzima ya Jumamosi February 28 alikuwa pamoja na 
baba yake wakazunguka maeneo mbalimbali na baadaye wakarudi nyumbani 
akiwa mzima kabisa, hali ilibadilika muda mfupi baadaye ambapo 
walipofika njiani wakati wakimpeleka Hospitali alikata kauli.
Mazishi ya Mbunge huyo yatafanyika Mkoa 
wa Ruvuma ambako mtoto huyo wa Marehemu amesema baba yake aliagiza kama 
akifariki azikwe huko.
 
No comments:
Post a Comment