Kisa cha mtoto kuuawa na mjomba wake, watu wakamuua mjomba.

Watu hao waliokuja eneo hilo walimkuta
mjomba huyo akiwa amemuua mtoto huyo, wakaamua kumpiga na yeye mpaka
akafariki, baadaye wakamchoma moto.
Baba wa kijana huyo ambaye ni mjomba wa mtoto huyo amesema kijana huyo alikuwa na matatizo ya kifafa kwa muda mrefu.

Fundi aliyekuwa eneo la tukio amesema
mtoto huyo alifika eneo hilo wakawa wanazungumza nae, ghafla akatokea
mjomba wake akiwa na fimbo akaanza kumuuliza maswali akakimbilia ndani
kutafuta mlango wa kutokea, akamkimbiza na kumkamata wakasikia kelele na
kuingia ndani wakamkuta kijana huyo akiwa na kisu mkononi na sururu
akimchinja mtoto huyo, wakaanza kupiga kelele kuomba msaada wananchi
walipofika wakaanza kumpiga na kisha kumchoma moto.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment