Kumbe uigizaji uliwahi kumletea mzozo Muhogo Mchungu kisa mke wa mtu?
Muigizaji mkongwe Muhogo Mchungu leo
alikuwa mgeni kwenye moja ya kituo cha Radio na kuzungumza kuhusu sanaa yake, wapi
anapenda na wapi hapendi kuingiza.. Ishu ya kuigiza kama baba mwenye
nyumba ndogo kumbe ni waandaaji wa filamu hizo wanapenda kumpanga kwenye
nafasi hizo.
Akizungumzia kuwahi
kukutana nayo kuna siku walienda Shinyanga kwenye michezo ya jadi
kitaifa, akakutana na dada mmoja ambae alitaka kufanya filamu wakawa
wanawasiliana.
Baadaye mume wa dada huyo alimtuhumu
Muhogo kuwa na uhusiano na mpenzi wake baada ya kukuta message
walizokuwa wanatumiana, japo alijaibu kumuelekea kuwa walikuwa kwenye
majadiliano kuhusu filamu mwanaume huyo hakuelewa.
Kuhusu watu ambao anapenda kucheza nao filamu amesema anaelewana sana na Bi Staa kutokana na kwamba walianza wote sanaa.
Muhogo Mchungu amesema anaipenda sana tamthilia ya Fukuto na filamu ya Kigodoro.
No comments:
Post a Comment