Monday, March 16, 2015

MWANAFUNZI ALISHWA BANGI BADALA YA CHOCOLATE

Ilikuwa zawadi ya chocolate, lakini kilichomo ndani ni story tofauti..

IMG_1619_2Mwanafunzi mmoja ambaye umri wake ni miaka 17 Marekani amelazwa baada ya kupata ugonjwa wa kupooza baada ya kula chocolate aliyonunuliwa na marafiki zake ambao wanasoma darasa moja katika shule ya Benjamin Banneker High School huko Brooklyn.
Mwanafunzi huyo Danieel Buchanan aliletewa chocolate na wanafunzi wenzake ambayo walikula wote, muda mfupi baadae hali ilikuwa mbaya akapelekwa Hospitali ambapo muda mfupi baadae mtoto huyo aliruhusiwa kuondoka na wazazi wake.
Muda mfupi baadaye hali ya Buchanan ilibadilika tena, akashindwa kuongea, kutembea, kula na miguu yake kupooza.. Mama yake akaamua siku ya pili yake kumpeleka Hospitali ya Mount Sinai ambapo baada ya kufanyiwa vipimo ilionekana kuwa kwenye chocolate aliyokula kulikuwa na bangi, rafiki ambaye alimpa Buchanan chocolate hiyo alisimamishwa shule anayosoma huku Polisi wakiendelea na upelelezi.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment