Isikie hii ya ndege iliyolazimika kuhairisha safari ikiwa angani na kurudi ilipotoka…
Tunafahamu
kuwa ndege hulazimika kutua gafla ikiwa katika safari yake pale tu
ambapo kunatokea hitilafu ikiwa angani na kusababisha kutua hata kama
haijamaliza safari yake.
Unaweza
ukadhani si jambo rahisi lakini hii ni ya kweli imetokea baada ya ndege
moja ya shirika la ndege la British Airways kulazimika kutua kufuatia
harufu mbaya iliyokuwa ikitokea ndani ya choo.
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea Heathrow Uingereza kutoka Dubai safari ambayo kwa kawaida huchukua saa saba.

Rubani wa ndege hiyo alimwita msimamizi
wa wahudumu wa ndege hiyo ndipo wakagundua kulikuwa na harufu mbaya ya
choo katika safari yao iliyotokea ndani ambayo inaweza kuhatarisha afya
zao.
Alisema ilikuwa tayari nusu saa tangu
waanze safari na kulazimika kurejea Dubai na hakukua na ndege mbadala
ya kuwarejesha London hivyo kusubiri kwa zaidi ya saa 15 .
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment