Yamoto Band show nyingine nje? Kingwendu anatamani kwenda
Jana alisikika Nikki wa Pili
akizungumzia campaign yake kuhimiza mwamko wa watu kwenye uchaguzi Mkuu
wa mwaka huu, kundi la Watanzania wanaoishi Marekani wameamua kuungana
na kutengeneza wimbo ambao unahamasisha Watanzania kufanya uchaguzi wa amani
mwaka huu na kuchagua viongozi wanaowataka.
Kundi hilo linaitwa DMV All Star wamesema wana mpango wa kusafiri na kuja Tz kwa ajili ya kupiga kura pamoja na kuhimiza watu kushiriki kuchagua viongozi.
Yamoto Band
wameanza kuingia kwenye Headlines za wasanii Bongo wanaopata mashavu ya
show nje ya Tz, walikuwa Uingereza wakapiga show, siku chache zijazo
watapanda pipa kuelekea Muscat kwa ajili show pia wakiwa na Ommy Dimpoz, Mkubwa Fella amesema baada ya Muscat
kuna show nyingine kubwa zaidi ambayo itafuatia lakini itafahamika show
hiyo wanaenda kupiga wapi baada ya masuala ya viza kukaa sawa.
Kingwendu
ni mmoja ya wachekeshaji maarufu Bongo, leo kasikika pia akizungumzia
nchi ambazo ana hamu sana ya kuzitembelea kama akijaaliwa kupata nafasi
hiyo.
Baadhi ya nchi ambazo anatamani sana kuzitembelea ni pamoja na Congo maeneo ya Kinshasa, Maputo Msumbiji, Marekani na Uingereza.
Ziko story nyingi sana kwamba Ulaya hamna mchanga, hamna miti, jamaa anatamani aende ili nae aone hivyo vitu kwa macho yake.
Kuna taarifa ya majonzi toka Uganda, inahusu msiba wa msanii wa Reggae AK47 ambaye ni mdogo wa Jose Chameleone ambaye amefariki jana usiku baada ya kuanguka bafuni.
Ripota kutoka Uganda amesema familia
bado haijapanga kuhusu mazishi kwa kuwa wanamsubiri kaka wa Marehemu
awasili kutoka Marekani ili ashiriki mazishi ya mdogo wake huyo.
Baba wa AK47
anahisi kifo cha mtoto wake sio cha mazingira ya kawaida kwamba
ameanguka tu bafuni, kuna kitu tofauti ambacho yeye anakihisi japo
hajazungumzia kuhusu hilo kwa sasa.
Nyumbani kwa baba wa msanii huyo
kumefurika watu wengi ambapo Polisi wamelazimika kuwepo katika mazingira
ya nyumba hiyo ili kuhakikisha usalama unakuwepo.
No comments:
Post a Comment