TANGA KUMEKUCHA

Saturday, March 14, 2015

NILIJUA NIMEUA SEHEMU YA KWANZA

HADITHI
 
NILIJUA NIMEUA (1)
 
 
Kujuana kwangu na Halima kulikuwa kwa bahati sana. Awali sikuwa na mawazo kabisa ya kwamba nitakuja kukutana na kusuhubiana na msichana mrembo kama yeye.
 
Siku moja ambayo ninaikumbuka hadi leo nikiwa kwenye teksi yangu maarufu kama Majombi Teksi, nilikuwa ninatoka hospitali ya Bombo ambayo ni hospitali ya mkoa iliyoko Tanga.
 
Nilikuwa nimempeleka mama mmoja mjamzito kutoka hospitali ya Ngamiani. Mama huyo alipelekwa hospitalini hapo kujifungua lakini kutokana na umri wake kuwa mkubwa madaktari wakaamua wamhamishie Bombo.
 
Ndugu zake waliiona teksi yangu ambayo huiegesha karibu na hospitali hiyo kusubiri abiria, wakanikodi niwapeleke Bombo.
 
Wakati narudi kutoka Bombo mvua ilikuwa imeanza kunyesha. Nikaona msichana aliyekuwa amesimama pembeni mwa barabara akinipungia mkono kwa bidii huku akitota na mvua. Ilikuwa wazi kuwa mvua ilimkuta ghafla njiani na mahali alipokuwa hapakuwa na sehemu ya kujisitiri. Mimi kama dereva wa teksi nilishukuru kwa hilo.
 
Nilipunguza mwendo na kuisimamisha gari pembeni mwa barabara. Nilikuwa nimempita kidogo. Alipoona teksi imesimama aliifuata haraka akafungua mlango wa nyuma na kujipakia.
 
“Unakwenda wapi?” nikamuuliza.
 
“Nipeleke barabara 20 nyuma ya CCM” akaniambia. Sauti yake ilikuwa nyembamba na nyororo.
 
Alijisogeza katikati ya siti ili kukwepa upepea wa mvua uliokuwa ukipenya kwenye dirisha. Nikawa namuona vizuri kwenye kioo cha gari cha kutazamia nyuma.
 
Wakati naiondoa teksi nilikuwa namkodolea macho kupitia kwenye kioo hicho bila mwenyewe kujua.
 
Uso wake ulikuwa umenywea kutokana na fadhaa ya kutoswa na mvua lakini alikuwa na sura jamali ya macho makubwa aliyoyapaka wanja mzito. Juu ya macho yake pembeni mwa kopi alikuwa amepaka rangi iliyoendana na nguo aliyokuwa amevaa.
 
Pua yake ilikuwa ndefu na midomo ya wastani aliyokuwa ameipaka rangi hafifu ya waridi.
 
Nilimuona tangu alipokuwa amesimama alikuwa mrefu , mweupe na mwenye mwili wa wastani. Vazi alilokuwa amevaa, dera la maua ya rangi ya bluu ya kung’aza na ushungi wake aliokuwa ameutanda kichwani vilimfanya aonekane alikuwa msichana aliyejistahi sana.
 
“Mvua za ghafla namna hii zinatuharibia bajeti” akasema kwa sauti ya kuchukia.
 
“Kwanini?” nikamuuliza huku nikitia gea ya pili.
 
“”Mahesabu yangu yalikuwa kupanda bodaboda, sasa nalazimika nipande teksi ili nisitote, huoni kuwa nimeshaharibu bajeti yangu?’
 
Nikatoa tabasamu jepesi.
 
“Na sisi ndio tunapata riziki zetu, usiilani”
 
“Kwa hiyo unaiombea ili upate abiria kwa wingi eti?”
 
“Ndiyo maisha yalivyo. Huwezi kumwambia daktari unaombea watu waumwe ili waje kwako upate pesa, au huwezi kumwambia muosha maiti kuwa anafurahia watu wafe apate kazi. Yeye pia anasikitika mtu akifa lakini ndiyo maisha. Kwa mmoja kukienda kilio kwa mwingine kunakwenda furaha”
 
“Sawa bwana, umeshinda wewe”
 
Nikacheka. “Sasa unataka nikalie wapi dadangu kama sio kwenu?”
 
“Basi nipunguzie kidogo”
 
“Ni shilingi elfu tano tu”
 
“Ndiyo nakwambia nipunguzie, nitakupa elfu tatu”
 
Nikatikisa kichwa. Tabasamu lililokuwa usoni kwangu likatoweka. Sikutaka masihara yaingie kwenye kazi yangu. Teksi ile haikuwa mali yangu. Nilikuwa nimeajiriwa na mwenyewe alitaka nimpelekee shilingi elfu ishirini kila baada ya masaa ishirini na nne, bila kujali nimeingiza kiasi gani.
 
“Elfu tano ndio kima chetu, haipungui. Petroli imepanda sana” nikamwambia.
 
Wakati nampa jibu hilo simu yake iliyokuwa kwenye mkoba wake ilianza kuita. Akaitoa na kuipokea.
 
“Ninakuja, nisubiri” akasema kwenye simu.
 
Alisikiliza kidogo kisha akaendelea.
 
“Nimekodi teksi…poa…”
 
Akairudisha simu kwenye mkoba.
 
Nilikuwa nimetokea kwenye eneo la Tangamano. Mvua ilikuwa imezidi. Eneo hilo lilikuwa halipitiki kwa maji. Niliipitisha teksi yangu kwa taabu kwa kutumia gea kubwa. Mpaka nakaribia kufika stendi ndio nilipata afadhali kidogo.
 
Nikaendelea na safari hadi barabara 20. Nilikata kulia, nikalipita jingo la ofisi ya CCM na kuingia mtaa wa nyuma yake. Mtaa huo ulikuwa umejaa matope.
 
“Twende kwenye nyumba ile pale” abiria wangu akaniambia.
 
Alinionesha nyumba iliyokuwa katikati ya mtaa huo upande wa kulia. Ilikuwa nyumba ya kawaida iliyoonekana kuwa tulivu.
 
Niliposimamisha teksi, msichana aliniuliza.
 
“Nikupe kiasi gani?”
 
“Elfu tano”
 
Nikadhani ataanza tena kulalamika kutaka kupunguziwe kiasi cha pesa. Lakini haikuwa hivyo, alifungua mkoba wake akatoa noti ya shilingi elfu tano na kuniambia.
 
“Shika”
 
Niligeuka nikaipokea kisha nikamfungulia mlango.
 
Akashuka haraka na kukimbilia kwenye baraza ya ile nyumba. Wakati anabisha mlango nikaiondoa teksi.
 
Nilirudi katika egesho langu lililokuwa karibu na hospitali ya Ngamiani.
 
Nililipendelea egesho hilo kwa maana. Kwanza lilikuwa karibu na hospitali ambapo mara kwa mara kunakuwa na wagonjwa wanaohitaji huduma ya teksi. Pili nilikuwa peke yangu na tatu kulikuwa na mahoteli mengi yaliyokuwa karibu na hapo na kufanya nipate wateja wengi.
 
Wakati naliegesha gari nilisikia mlio wa simu ndani ya gari. Nikashituka na kudhani ilikuwa simu yangu. Lakini niligundua haikuwa simu yangu. Simu yangu haikuwa na mlio kama huo  niliousikia.
 
Je mlio huo ni wa simu ya nani? Usikose kuendelea na hadithi hii mtu wangu kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com








Imechapishwa na Unknown kwa 10:56 PM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Time

 Time in Tanga

Total Pageviews

My Blog List

Blog Archive

  • ►  2014 (563)
    • ►  November (97)
    • ►  December (466)
  • ▼  2015 (3131)
    • ►  January (417)
    • ►  February (332)
    • ▼  March (351)
      • HADITHI SEHEMU YA (3)
      • 126 WAUWAWA MSIKITINI YEMEN
      • SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO, MARC 21
      • YANGA YALIPIZA KISASI CHA SIMBA
      • UAMINIFU NDANI YA NDOA UKIMSALITI MWENZA KIFUATACH...
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHA BLOG
      • ARSENAL RAHA
      • SOMA MAKUBWA YALIYOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO,TZ
      • UDANGANYIFU WA MAJIBU YA KITIHANI INDIA NAO WAMO
      • MAHAKAMA YAMWACHIA CHRIS BROWN
      • AJIFUNGUA WATOTO WAWILI NDANI YA MWAKA MMOJA
      • AZAM MAMBO SAFI, YAISHINDA COASTAL UNION YA TANGA ...
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHA BLOG
      • BARAZA LA UONGOZI CHADEMA MKOA LAWASIMAMISHA VIONG...
      • BARCELONA YAIADHIBU REAL MADRID
      • SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO, MARCH 2...
      • BECKHAM ANA KITU KINGINE NJE YA SOKA
      • OSCAR PISTORIUS AGEUKA MWANASOKA GEREZANI
      • AKAMATWA NA MADAWA YAKULEVYA, ISHU ALIPOYAFICHA
      • ATAKA KUMTOA UHAI MAMA YAKE , KISA KUPOKWA SIMU YA...
      • MWANAMKE AFANYA KAZI YA KUOSHA MAITI KWA MIAKA MIT...
      • MSICHANA AFIA KWA MPENZI WAKE, KILICHOFUATA NI ISHU
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHABLOG
      • NILIJUA NIMEUA SEHEMU YA (4)
      • SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO,MARC 24 TZ
      • MKUU WA MKOA WA TANGA, SAID MAGALULA AWAZINDUA WAG...
      • MCHINA AWEKA SHERIA KALI KUINGIA MGAHAWANI MTU MWE...
      • CHAMA CHA SOKA ENGLAND YATAKA KUWABANA WANASOKA WA...
      • FUMANIZI KATIKA SIMU
      • WEMA AIPA TANO MITANDAO YA KIJAMII
      • BREKING NEWS
      • SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO MARCH 25 TZ
      • VIMBWANGA VYA WALIMWENGU
      • JAMANI----NI THIERRY HENRY HUYO
      • KIGEUGEU
      • MAFURIKO TANGA
      • HANDENI NI KILIO CHA MAJI KILA KONA
      • UOKOZI NDEGE ILIYOPOTEA UNAENDELEA
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHABLOG
      • SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA NA MAGAZETI YA LEO, TZ
      • KAZI INAENDELEA
      • JE, WAJUA RONALDO NDIE ANAELIPWA FEDHA NYINGI ZAIDI
      • JE, WAJUA RONALDO KUWA NDIE ANAELIPWA PESA NYINGI
      • MAITI YANZINDUKA IKIWA MOCHWARI
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHA BLOG
      • NI VILIO TU, AJALI YA NDEGE YA GERMANWINGS
      • NYUMBA TATU ZA NGUVU
      • KINGINE KUHUSU MGAHAWA WA KICHINA KULE NAIROBI
      • MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO, MARCH 27 TZ
      • KISANDUKU CHEUSI NDEGE ILIYOANGUKA CHAPATIKANA
      • BABU TERYY ASAINI MKATABA MWAKA MMOJA CHELSEA
      • UFISADI KENYA WAMUMIZA KICHWA KENYATA
      • KUPIGANA MABUSU INDIA IMEKUWA GUMZO
      • SIERRA LEONE YAUMIZA KICHWA NA UGONJWA WA EBOLA
      • WANANCHI WASUSIA MAITI NA KUIPELEKA KITUO CHA POLISI
      • MAADHIMISHO SIKU YA KUTUNDIKA MIZINGA , HANDENI
      • RC , MAGALULA ACHOSHWA NA UCHOMAJI MOTO MISITU
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHABLOG
      • YAMEISHA
      • SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO, MARC 28 TZ
      • TUMEYAMALIZA
      • VIMBWANGA VYA WALIMWENGU
      • KUMBE JAMES BOND BADO WAMO ????
      • WAREMBO 10 DUNIANI
      • KUMBE NAE MANNY PACQUIAO YUMO
      • SIMU YA MAJANI
      • MACKERS WA MITANDAO WAIDIPI TUME YA UCHAGUZI NIGERIA
      • GWAJIMA AZIRAI WAKATI AKIHOJIWA NA POLISI
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHABLOG
      • NILIJUA NIMEUWA SEHEMU YA (4)
      • SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO,MARCH 29 TZ
      • CHALSEA YAMUWINDA BALE
      • ATENGEWA BREAKFAST YA PANYA
      • KONGAMANO LA UZAZI, ZANZIBAR, JE KUPANGA UZAZI WA ...
      • CHANZO CHA KIFO CHA ABDUL BONGE HIKI HAPA
      • KUTOKA MSIBANI KWA ABDUL BONGE
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMECHABLOG
      • UNAPENDA KUWA NA MJENGO KAMA HUUU, HEBU CHEKI
      • SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO TZ
      • TUNASHANGAAA, VAN GAAL AIBUKA KIDEDEA
      • JAMES BOND ADAIWA KUWA NI MBAGUZI WA RANGI
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMECHA BLOG
      • WAHOJI OBAMA KUSUSA KWENDA KWAO, KENYA
      • MTOTO ACHUKUA BASTOLA NA KUMMIMMINIA KAKA YAKE
      • KUMBE NDEGE YA AUSTRALIA ILIYOUA WATU 150 RABANI A...
      • SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO MARC 31 TZ
      • HII NDIO DUNIA NA MAAJABU YAKE
      • UNA PESA" NUNUA HII BASI
      • WANYAMA WATUMIKA KUPELEKA UJUMBE
      • MAITI YAPATA AJALI WAKATI IKIPELEKWA KUZIKWA
      • AANDIKA BARUA KWA RUBANI BAADA YA KUFIKA SALAMA
      • MGENGO WA MIKE TYSON KUWA KANISA
      • ANA MIAKA 56 WATOTO 40
      • MAYWEATHERER NA MANNY WAWAGAWA WAMAREKANI
      • ABDUL BONGE AZIKWA KWAO
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHABLOG
      • MUHAMMADU BUKHARI AIBUKA KIDEDEA NIGERIA
      • MAMBO YA MAY 1 HAYOO
      • MAJIJI 10 YENYE FOLENI KUBWA DUNIANI
      • MTOTO WA MIAKA MIWILI AVUNJA RECORD YA KULENGA SHA...
    • ►  April (308)
    • ►  May (263)
    • ►  June (255)
    • ►  July (260)
    • ►  August (246)
    • ►  September (237)
    • ►  October (210)
    • ►  November (142)
    • ►  December (110)
  • ►  2016 (1913)
    • ►  January (121)
    • ►  February (102)
    • ►  March (131)
    • ►  April (198)
    • ►  May (196)
    • ►  June (197)
    • ►  July (197)
    • ►  August (186)
    • ►  September (159)
    • ►  October (160)
    • ►  November (138)
    • ►  December (128)
  • ►  2017 (562)
    • ►  January (134)
    • ►  February (106)
    • ►  March (113)
    • ►  April (77)
    • ►  May (72)
    • ►  June (11)
    • ►  September (1)
    • ►  October (36)
    • ►  November (10)
    • ►  December (2)
  • ►  2018 (1)
    • ►  February (1)
Picture Window theme. Powered by Blogger.