Huenda familia ikaamua kingine kuhusu mtoto wa Whitney Houston
Ni zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu Bobbi Christina adondoke
bafuni na kupoteza fahamu, japo familia yake imekuwa ikitoa taarifa
kwamba hali yake inaendelea vizuri zipo taarifa zinazosema kuwa hakuna
dalili yoyote ya msichana huyo kupata nafuu.
Familia yake, watu wa karibu wamekua wakitumia muda mwingi kumfanyia maombi msichana huyo.
Familia
yake imepanga kukutana mwishoni wa wiki hii ili kuzungumzia hali ya
msichana huyo ambaye mpaka sasa anatumia mashine kupumua na huenda
wakafanya uamuzi wa wa kumtoa kutoka kwenye mashine hiyo ya kupumulia.
Bibi wa Christine ambaye ni mama mzazi wa Whitney Houston, amesema ni bora mjukuu wake akatolewa mashine hiyo, baba yake mzazi Bobbi Brown ni kama yuko njiapanda juu ya nini aamue.
Kwa mujibu wa daktari anayesimamia matiibabu ya binti huyo amesema hadi sasa hakuna dalili yoyote ya matumaini ambayo Bobbi Christina ameonesha tangu alazwe hospitalini hapo.
Hakuna story itakayokupita , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment