Baba kaamua kumchoma mtoto wa jirani yake kulipiza kisasi

Mtoto huyo amesema alikuwa anatoka nje
akiwa amebeba sufuria la moto, mtoto mmoja akatokea akiwa anakimbia na
kugongana naye, mtoto huyo akaumia kwa bahati mbaya kichwani.
Baadae watoto waliokuwa uwanjani
wanacheza, baba wa mtoto aliyeunguzwa alimuita mtoto ambaye alimumiza
mwanae na kwenda naye nyumbani kwake, akaweka kisu jikoni na kumchoma
nacho sehemu mbalimbali mwilini kama kulipiza kisasi.
Majirani baada ya kugundua tukio hilo
waliamua kwenda kushtaki Serikali za mitaa kutokana na mama ambaye mtoto
wake amechomwa kulipiza kisasi kuogopa kutoa taarifa akihofia kufukuzwa
kwenye nyumba hiyo aliyopangishwa na baba ambaye kamchoma mwanae.
Polisi walifika eneo hilo na kumkamata mtuhumiwa.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment