Thursday, March 19, 2015

VIUNGO VYA BINADAMU VYAKUTWA NDANI YA GARI LA MHUBIRI, KULE KENYA

Uliipata hii ya gari la Mhubiri kukutwa na viungo vya binadamu Kenya?

police-line-do-not-cross
Mwanaume mmoja nchini Kenya amekamatwa akiwa na mfuko uliojaa vitu vilivyosadikiwa kuwa ni viungo vya binadamu.
Baada ya mahojiano na Polisi jamaa huyo alisema kwamba vitu hivyo sio vyake, ila ni vya mhubiri mmoja eneo la Magongo.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya gari alilokuwa akiendesha kuharibika na kusimama ili kulirekebisha, walinzi waliokuwa kwenye duka moja karibu na eneo hilo walisikia harufu kali na kuamua kumpekua ambapo walimkuta na mfuko huo uliokuwa umejaa damu.
Polisi walifika na kumkamata dereva huyo, walipomhoji aliwaambia gari na vitu hivyo vinamilikiwa na mhubiri Andrew Chobe, Polisi walimtafuta mhubiri huyo ambaye amekiri kwamba vitu hivyo ni vya kwake, alipewa na familia moja ambayo aliifanyia maombi na ikampatia viungo hivyo ili kwenda kuvitupa baharini.
Polisi wamechukua viungo hivyo na kuvipeleka katika Maabara ili vichunguzwe.

No comments:

Post a Comment