Man City kuwaondoa wachezaji hawa kwenye kikosi chake msimu huu.
Kipigo cha Manchester City dhidi ya Barcelona cha bao 1-0 huenda ikiwa moja ya sababu ya kocha mkuu wa timu hiyo Manuel Pellegrini kuamua kuwaondoa katika orodha yake baadhi ya wachezaji wa kikosi chake akiwemo Yaya Toure.
Mabingwa hao wa ligi ya Uingereza wamepanga kuwauza baadhi ya nyota wake msimu huu akiwemo Yaya Toure, Gale Clichy, Pablo Zabaleta,Jesus Navas, Fernandinho, Steven Jovetic na Edin Dzeko.
Man City alishindwa kutinga hatua ya robo fainali dhidi ya Barcelona
katika mechi ya kombe la klabu bingwa Ulaya na kocha wake amethibitisha
kwamba mabadiliko makubwa yatafanyika ndani ya klabu hiyo.
Hakuna story itakayokupita , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment