Monday, March 16, 2015

WAHABESHI 64 WAKAMATWA WAKIWA WAMEFICHWA MSITUNI DODOMA

WAHAMIAJI HARAMU 64 RAIA WA ETHIOPIA WAKAMATWA MKOANI DODOMA



Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Wananchi imewakamata Wahamiaji haramu 64  raia wa nchi ya ETHIOPIA (Wahabeshi) katika Kijiji cha KIDOKA, Kata ya KIDOKA, Tarafa ya GOIMA, Wilaya ya na CHEMBA  Mkoa wa DODOMA, mmoja kati yao alikutwa akiwa amefariki  aliyetambuliwa kwa jina moja la TAJIRU anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 – 30. Watu hao walikuwa wakisafirishwa kwa Lori aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa likiendeshwa na OTHMAN YUNUS MTEKATEKA, miaka 45, na Mkazi wa ILALA Jangwani  jijini Dar es Salaam akitokea Moshi - Kilimanjaro kwenda mkoani Mbeya.

 
Watu hao walionekana dhaifu, walikuwa wakila mahindi mabichi na wengine wakiomba kwa wanakijiji waliokuwa wakipita maeneo jirani msaada wa chakula na maji ya kunywa kwa ishara,  kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kuzungumza Kiswahili wala  Kiingereza.





Sehemu ya Wahamiaji haramu 64  raia wa nchi ya ETHIOPIA (Wahabeshi) wakiwa hoi na kupatia huduma za kiutu zikiwemo chakula na matibabu.

No comments:

Post a Comment