Mkusanyiko huu wa Stori 10 kutoka magazetini unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga,kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi sita, Pia kituo kinatoa English Cozz kwa wakubwa na wadogo. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 771746
Mapya yanazidi kuibuliwa juu ya sakata linaloiandama Kampuni ya Reli Limited (TRL) ya uingizaji mabehewa feki nchini, sasa ikifahamika kuwa hata Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), haikushirikishwa kwenye manunuzi hayo.
Kufichuka kwa ukweli huo, ndiko sasa
kunaongeza hali ya wasiwasi ndani ya TRL na kuna uwezekano mkubwa sakata
hilo litaibua mjadala katika mkutano wa 19 wa Bunge unaotarajiwa kuanza
kesho mjini Dodoma.
Ukweli huo uliwekwa wazi mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Luaga Mpina, wakati wa kikao cha kamati yake na PPRA.
Mpina alitoboa siri hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao baina ya kamati yake na PPRA.
Alisema kamati yake iliwahoji PPRA
kuhusu ushiriki wao kwenye ununuzi wa mabehewa hayo na kubaini kuwa
mamlaka hiyo haikushirikishwa.
“Tunashangaa
kwamba hata PPRA hawakushirikishwa kwenye mchakato wa ununuzi wa
mabehewa hayo. Hadi sasa ninapozungumza hawajawahi kuitwa kushuhudia
mabehewa 150 yaliyobainika kuwa ni feki,” Mpina.
Mpina ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa,
alisema hali hiyo inaonyesha mambo kufanywa kinyume cha taratibu katika
mchakato mzima wa ununuzi wa mabehewa hayo, hali aliyosema imechangia
kuingiza hasara serikali kwa kununua mabehewa feki.
Ili kulishughulikia suala hilo sawa
sawa, mbunge huyo alisema kamati yake inatarajia kukutana na uongozi wa
PPRA chini ya mkurugenzi wake, Laurent Shirima Ijumaa wiki hii mjini
Dodoma, kwa ajili ya kupata taarifa zaidi kuhusu ununuzi wa mabehewa
hayo feki.
Wakati huo huo, kamati iliyoudwa na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, imewasilisha taarifa ya uchunguzi wake kwa Bodi ya Wakurugenzi wa TRL kama walivyoagizwa na Waziri wa sasa wa Uchukuzi, Samuel Sitta, ambaye anatarajiwa kukabidhiwa ripoti hiyo.
NIPASHE
Serikali imesema kuanzia kesho kituo cha
mzani cha Kibaha kitafungwa na magari yote yataendelea kupimwa kwenye
kituo kipya cha Vigwaza kilichopo Mkoa wa Pwani.
Pia inatarajia kutumia Sh. bilioni 8 kujenga mizani mipya mitano ya kisasa katika maeneo mbalimbali ikiwamo eneo la Mikese, Dumila, Nala mkoani Dodoma, lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari katika maeneo ya mizani.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale, aliyasema hayo wakati wa utoaji wa taarifa juu ya kuanza kutumika kwa mzani mpya wa Vigwaza.
Mfugale alisema kesho Serikali
itakifunga rasmi kituo cha mzani cha Kibaha na magari yote yataendelea
kupimwa kwenye kituo kipya cha Vigwaza.
Alisema kituo hicho ni cha kisasa chenye mtambo wa kuchambua magari yaliyozidisha uzito yakiwa yanatembea.
Pia, alisema kituo hicho kina mzani mkubwa unaoweza kupima gari lote kwa mkupuo.
“Aidha
barabara za kuingia kwenye mzani huo wenye urefu wa kilomita 1.8
zimejengwa kwa zege lenye uwezo wa kudumu kwa miaka 50 na una uwezo wa
kupima gari moja kwa sekunde 30 badala ya dakika 1.5 kwa mzani wa zamani,” Mfugale.
NIPASHE
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ametoa siku saba kwa Hospitali ya TMJ,
Dar es Salaam, kuhakikisha inajenga mtaro wa kupitisha maji machafu ili
kuondokana na majitaka hayo kuingia kwenye mitaro mipya inayojengwa.
Alisema kama hospitali hiyo itapuuza
agizo hilo, ndani ya siku saba, serikali itachukua hatua stahiki ikiwamo
ya kuzuia kutoa huduma.
Makonda alitoa kauli hiyo alipotembelea
kwenye maeneo ya Mikocheni kukagua miundombinu ya barabara na mitaro
inayojengwa ili kudhibiti athari za mvua zinazotarajia kunyesha wakati
wowote.
Makonda, alishuhudia mtaro wa majitaka
ya hospitali hiyo ukitiririsha uchafu kuelekea kwenye mitaro mipya
inayojengwa hali iliyosababisha mitaro hiyo kujaa taka kabla ya
kukamilika kwake.
Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Mbaraka Mkwiya,
alisema miradi ya ujenzi wa mitaro ya maji taka kwenye bonde la mpunga
unagharimu takribani Sh. bilioni sita na barabara tano za mitaa ya
Mikocheni na Msasani ambazo zitagharimu Sh. bilioni 3.3 ambayo yote,
inatarajia kukamilika miezi michache ijayo.
MWANANCHI
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
amewaaga wapigakura wake kuwa hatakuwa tena mbunge wao, akisema kuwa
kesi ya dhidi ya Chadema ilitupwa na Mahakama Kuu kutokana na baadhi ya
majaji kutajwa kwenye kashfa ya escrow.
Chadema ilimvua Zitto uanachama saa
chache baada ya Mahakama Kuu kutupa shauri lake alilofungua akitaka
chombo hicho cha sheria kimlazimishe katibu mkuu wa chama hicho kumpa
nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua nyadhifa zote,
huku akifanikiwa kupata amri ya muda ya kuizuia Chadema kumjadili.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Kata ya Mwandiga mkoani Kigoma jana, Zitto alisema hatakuwa
mbunge wa jimbo hilo baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, na
akatumia fursa hiyo kueleza safari yake ya kisiasa ndani ya Chadema na
mtazamo wake baada ya kufukuzwa uanachama.
“Nimejifunza
mengi nikiwa mbunge. Katika utumishi wangu kwenu, bungeni nimejifunza
namna nchi yetu inavyoendeshwa. Katika kujifunza huko kuna mambo kadhaa
nimefanya ya kujivunia na mengine ni makosa,” alisema Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chadema.
“Nimejifunza
kuwa mzalendo zaidi kwa nchi yangu na kuwatumikia watu wa nchi hii.
Ndiyo maana hamkunisikia tu nikitetea watu wa Kigoma pekee, bali watu
maeneo mengine ya nchi yetu na makundi mbalimbali ya kijamii.”
Alisema safari yake ya ubunge ilikuwa ngumu yenye mafunzo makubwa na imemfanya apevuke kifikra na kupata mafunzo.
Awali, akizungumza na waandishi wa habari, Zitto alisema: “Bado nina nia ya dhati ya kuendelea kuwatumika Watanzania kama mwakilishi wao kupitia jimbo lolote nchini.
MWANANCHI
Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
wiki ijayo wanatarajia kuzindua treni ya mizigo ‘block train’ kutoka
jijini hapa kwenda nchi wanachama kwa kutumia reli ya kati.
Uzinduzi huo wa treni zenye mabehewa 20
hadi 21 utakwenda sambamba na mkutano wa marais wa EAC utakaofanyika
Machi 25-26, Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta
aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa uchukuzi wa
jumuiya hiyo na kuongeza, uzinduzi huo utaanza na safari ya kwenda
Burundi na Rwanda kwa siku hiyo.
Sitta ambaye aliwahi kuwa Waziri wa
Afrika Mashariki kabla ya kuwa Waziri wa Uchukuzi, alisema treni hizo
pia zitasafari kutoka Dar es Salaam kwenda Uganda na DRC.
Akitolea mfano wa treni itakayo kwenda
Rwanda alisema ikitoka jijini hapa itaishia Isaka ambapo kutakuwa na
magari kwa ajili ya kubeba mizigo hiyo hadi Rwanda.
Alisema, utaratibu huo utakuwa endelevu
na unalenga kusaidia nchi wanachama kusafirisha mizigo mingi inayoingia
na kutoka nje ya nchi kwa haraka lakini hasa zile ambazo hazijapakana na
bahari.
Mbali na uzinduzi huo, Sitta alibainisha
kwamba wakuu hao watakuwa na mkutano kwa ajili ya kujadili namna ya
kuboresha usafiri kwa ukanda wa kati.
Baada ya mkutano wa kwanza, utafuatiwa na mkutanao wa wakuu hao pamoja na wawekezaji.
Waziri wa Uchukuzi wa DRC Justine
Kanumba ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo, aliipongeza
Tanzania kwa hatua hiyo ambayo alisema itasaidia kurahisisha
usafirishaji kwa nchi wanachama.
MTANZANIA
Makundi ya watu wa kada mbalimbali yamezidi kutua nyumbani kwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), yakimtaka achukue fomu ya kuwania urais kupitia CCM muda utakapofika.
Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa
zamani, kwa wiki kadhaa sasa amekuwa akipokea wageni wa makundi
mbalimbali nyumbani kwake wakimtaka awanie nafasi hiyo ya uongozi wa juu
wa nchi.
Kutokana na joto hilo la urais ndani
CCM, jana makundi mawili ya wana CCM yalibisha hodi nyumbani kwa kada
huyo na kumshawishi kufanya hivyo pamoja na kumkabidhi fedha za
kuchukulia fomu.
Kundi la kwanza lilikuwa ni wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arumeru ambao
waliwasilisha ombi lao kwa mbunge huyo pamoja na kumkabidhi Sh milioni
moja za fomu.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Meru, John ole Saitabau, alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona Lowassa ana sifa zote za kuwania nafasi hiyo ya uongozi wa nchi.
“Sisi
tumekuja hapa kukushawishi uchukue fomu ya kuwania urais kupitia chama
chetu cha CCM… uwezo huo unao na Tanzania inakuhitaji,” Ole Saitabau.
Naye Mathias Manga, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC),
alisema zaidi ya asilimia 75 ya wajumbe wa NEC wanamshawishi Lowassa
awanie urais kwa sasa kutokana na sifa yake ya uchapakazi mbele ya
jamii.
Kundi la pili ambalo lilifika nyumbani
kwa Lowassa ni la marafiki wa Lowassa, Kanda ya Kaskazini, ambako zaidi
ya watu 500 kutoka kada mbalimbali wakiwamo walemavu wa macho na watu
wenye albino, walimkabidhi Lowassa Sh milioni 2.5.
Akisoma risala kwa niaba ya vijana
waliotoka katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara, Protas
Soka, alisema kwa sasa Watanzania wanamuhitaji Lowassa aweze kuliongoza
Taifa.
MTANZANIA
Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM) amewaomba
viongozi wa dini nchini kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali
wakiwamo wabunge ili wawatumikie wananchi kwa kutanguliza hofu ya Mungu.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati wa mazishi ya aliyekuwa mtawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Imiliwaa, marehemu Insetrud Maria.
Alisema viongozi wa dini wamekuwa
wakifanya kazi ya kuliombea taifa na watu wake lakini wanasiasa na
viongozi wa serikali wamekuwa wakiwatumikia wananchi kimwili hivyo kuna
haja ya viongozi wa dini kuendelea kufanya kazi ya kuwaombea viongozi.
“Maandiko
matakatifu yanasema; ‘enendeni duniani mkawafanye watu wote kuwa
wanafunzi wangu’…chama cha walimu hapa wamesema kuwa Sr.Maria alikuwa
mwalimu mzuri hivyo ni wazi alizifanya kazi zote, ya kiroho na kimwili,” alisema.
Kwa kutambua mchango wake alioutoa
duniani enzi za uhai wake, mbunge huyo aliahidi kujenga darasa katika
shule ya sekondari parokiani hapo kama njia ya kumuenzi zaidi.
Filikunjombe alisema kumbukumbu hiyo itakuwa kielelezo cha mchango wa Sr.Maria katika maendeleo ya Mkoa wa Njombe.
”
Sr.Instrud Maria mbali ya kazi yake ya utawa pia alikuwa ni mwalimu na
mchango wake katika shughuli zake ni mkubwa hivyo nawaombeni tumuenzi
kwa kujenga darasa moja ambalo litaandikwa jina lake kama kumbukumbu ya
sasa na baadaye,”alisema Filikunjombe.
DIRA
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
inalalamikiwa kuwa na unyanyapaa kwa wagonjwa wanaofika hapo ili kupata
huduma za afya kutokana na madaktari na manezi kuwa na kauli mbaya na
zisizofaa kwa wagonjwa.
Baadhi ya wagonjwa wanaopata huduma
katika hospitali hiyo inayotegemewa na Taifa ni tia maji tiamaji kwa
vile kwa vile ni mbovu na haifai na kusababisha kuishushia
hadhihospitali hiyo.
Katika hospitali hiyo wodi inayolalamkiwa zaidi ni ile ya mifupa MOI
kwa kudaiwa kujaza watu wengi hadi kulala chini, mashuka hayabadilishwi
kwa wakati na pia madaktari hawapiti kwa muda uliopangwa.
“Hii
hospitali ni bure kabisa nimemleta mgonjwa hapa hali ikiwa mbaya
kabisa,lakini daktari hakuwa na muda zaidi ya kuuliza nimejipanga vipi
ili mgonjwa wangu ahudumiwe vizuri, hadi nilipompa pesa ndipo mgonjwa
wangu akatibiwa, inasikitisha”.
Aliongeza kuwa hata alipomfikisha
mgonjwa wake kitengo cha MOI wauguzi waliokuwepo zamu siku hiyo
hawakumpokea wala kumjali mgonjwa na kuendelea na maongezi.
UHURU
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Itimila mkoani Simiyu, kimelitaka Jeshi la Polisi kusitisha msako wa waganga wa jadi wanaopiga ramli chonganishi.
Hatua hiyo imekuja huku Jeshi la Polisi
katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, likiwa katika msako mkali wa kuwakamata
waganga wa namna hiyo.
Mbali ya kulitaka jeshi hilo kusitisha
shughuli hiyo, pia CCM imetaka waganga hao wa jadi wapewe muda wa
kutosha ili wapatiwe leseni za kutambulika kwa kazi zao.
Agizo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Mohamoud Mabula,
wakati wa mkutano wa waganga wa jadi uliofanyikia katika viwanja vya
Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani humo mwishoni mwa wiki.
Mabula alimtaka Mkuu wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo,
aliyehudhuria mkutano huo, kusitisha shughuli hiyo kwa maelezo kwamba
baadhi ya waganga hao wa jadi wamekamatwa kutokana na kukosa leseni
lakini hawajihusishi na upigaji wa ramli.
Hata hivyo, alisema anatambua umuhimu wa agizo la Rais Jakaya Kikwete,
lakini kuhusu uendeshaji wa operesheni hiyo anaipinga kutokana na
waganga wengi kutopewa muda wa kujiandikisha ili kupatiwa leseni.
“Operesheni
hii inataka kutukumbusha operesheni kimbunga kwa wahamiaji haramu na
kukamata majangili. Operesheni hizi zimeondoka na viongozi wengi
wachapakazi, sasa hatutaki Chama kurudia makosa. Tunataka operesheini
zifanyike kwa amani na siyo kuwashtukiza watu,” Mabula.
Alieleza kuwa maagizo ambayo yamekuwa
yakitolewa na viongozi wao ngazi za juu kwa upande wa serikali, huwaweka
katika wakati mgumu viongozi wa Chama ngazi za mkoa na wilaya kutokana
na maagizo hayo kutekelezwa kwa nguvu.
“Sisi
kama Chama, tumeanza kupata malalamiko kutoka kwa wapigakura wetu.
Wanasema CCM inataka kuwafukuza waganga wa jadi…kwa hili hatukubali
tulalamikiwe tunachohitaji msako ufanyike lakini kwa amani na watafutwe
wapiga ramli tu na siyo waganga wote,” alisema.
Kauli hiyo ya kiongozi huyo wa CCM, ilipokewa kwa shangwe na waganga wa jadi zaidi ya 200 waliohudhuria mkutano huo.
HABARILEO
Mbunge wa Rufiji ambaye pia ni Waziri wa afya Dk. Seif Rashid juzi alichangia kuyaokoa maisha ya mama mjamzito Amina Bakari sliyesota porini kwa saa zaidi ya sita akisubiri usafiriwa kumfikisha hospitali ya Wilaya ya Utete kwa ajili ya kujifungua.
Kabla ya msaada huyo Mbunge huyo
aliyekuwa akifanya ziara katika jimbo lake alisema, Amina alikodi
pikipiki lakini baada ya kutembea umbali mrefu alishindwa kuhimili
mtikisiko wake na kuomba ashushe kwa kuwa uchungu ulikuwa umeongezeka.
Dereva wa bodaboda alikubali kumshusha katika eneo la Nyagolombe lakini kwa zaidi ya saa 6 mama huyo hakupata usafiri mwingine huku akihangaika kutokana na kushikwa uchungu.
“Lakini
tukiwa tumeshakata tama na kusubiri miujiza ya Mungu ajifungue
lilitokea gari na kulisimamisha kuomba msaada, kumbe ndani kulikuwa na
Mbunge wetu, hakuwa na hiyana akakubali kutusaidia kumkimbiza hospitali
ulikuwa umbali kama wa km 2o hivi ” alisema mwendesha bodaboda.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment