Bobi Wine safari hii kaimba Kiswahili wimbo wote mtu wangu- ‘Paradiso’
Watu
wengi wamekuwa wakidhani kwamba kwa muziki wa sasa hivi inabidi msanii
aimbe muziki wa mapenzi ili atoke, lakini zipo nyimbo ambazo hazina
ujumbe wa mapenzi na ni hit kali sana.. Vipi kuhusu ‘Mwana’ ya Ali Kiba? ‘Nani Kama Mama’ ya Christian Bella Feat. Ommy Dimpoz je?
Time ya Star kutoka Uganda ni sasa, Bobi Wine leo ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Paradiso’ .. Hapa anazungumzia umuhimu wa wazazi mtu wangu.
Afrika Mashariki inatambulishwa na lugha
ya Kiswahili, lakini mara nyingi tunaona wasanii wa Uganda wakiimba
lugha yao zaidi kuliko Kiswahili, time hii ‘Paradiso’ imeimbwa kwa Kiswahili mtu wangu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment