Ishu ya Ugaidi na headlines nyingine toka Chad kuhusu vazi hili !!
Shambulio la Kigaidi limetokea Chad
Jumatatu June 15 2015 katika Jiji la N’Djamena, watu 23 wakauawana
wengine zaidiya 100 wakapata majeraha makubwa.
Waziri Mkuu wa Chad, Kalzeube Pahimi Deubet amesema
mtu aliyelipua mabomu hayo alitumia vazi ambalo linavaliwa na wanawake
wa kiislamu ambalo linaziba mpaka usoni… Kingine kilichoamliwa leo ni
ishu ya kupigwa MARUFUKU kwa mtu yoyote kuvaa vazi hilo kwa mtu yoyote.
Agizo lililotolewa leo June 18 2015 ni
kwamba hakuna mtu yoyote anaeruhusiwa kuvaa vazi hilo popote ndani ya
Chad… Japo haijathibitika ni nani kahusika na Shambulio hilo, stori
mpaka sasa kutoka Chad zinataja sana kundi la Boko Haram kutokana na kitendo cha nchi hiyo kuisaidia Nigeria kupambana na Kundi hilo la wapiganaji.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment