Nyota wa Juventus matatani huko Chile baada ya kupata ajali..
Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Chile, Arturo Vidal
amekumbwa na mkasa ambao huenda atapenda kuusahau haraka iwezekanavyo
wakati akiwa na timu yake ya taifa ambayo kwa mwaka huu imekuwa mwenyeji
wa michuano ya Copa America.
Vidal ambaye
amekuwa kwenye kiwango bora tangu kuanza kwa michuano hiyo akiwa
amefunga mabao matatu kwenye mechi mbili amehusika kwenye ajali ya gari
ambayo imeelezwa kuwa yeye mwenyewe ndio alikuwa chanzo cha ajali hiyo.
Ripoti ya Polisi inaonesha kuwa Vidal alikuwa amelewa wakati akiwa anaendesha gari aina ya Ferarri na alisababisha ajali ambayo ilimsababishia majeraha madogo pamoja na mkewe ambae nae alikuwemo ndani ya gari hiyo.
Wote wawili waliwahishwa hospitalini
ambako wamekuwa wakitibiwa huku hali zao zikielezwa kuwa sio mbaya
kutokana na kupata majeraha madogo kwenye ajali hiyo.
Vidal
alikuwa akitoka kwenye klabu moja ya usiku baada ya wachezaji wa Chile
kupewa ruhusu ya kuondoka kambini baada ya mchezo wao dhidi ya Mexico.
Ripoti zaidi zinasema kuwa Vidal huenda akafukuzwa kambini ikiwa ni moja ya hatua za kinidhamu toka kwa kocha wa timu ya taifa ya Chile, Jorge Sampaoli ikithibitika kuwa aliendesha gari huku amelewa.
Nyota huyu anatarajiwa kupandishwa
Mahakamani hivi karibuni kujibu mashtaka ya kuendesha gari akiwa
ametumia kilevi na tayari ameporwa leseni yake.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment