Man City yatoa milioni 35 kumnunua Sterling
Klabu ya Manchester City imeimarisha ombi la kumsajili mashambulizi machachari wa Liverpool Raheem Sterling.
Mabingwa hao wa mwaka wa 2014 wametoa pauni milioni 35 sawa na dola milioni 55 kusmsajili. The Reds walikataa ombi la kwanza la kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 wakisema thamani yake ni pauni milioni 50.
Kuwepo kwa mchezaji huyo raia wa Uingereza katika soko kumetokana na nia yake ya kuondoka Liverpool .
Sterling alijiunga na Liverpool mwaka wa 2010 akitokea QPR kwa mkataba utakaomalizika mwaka wa 2017.
Hata hivyo alizua mjadala baada ya kuzima pendekezo la nyongeza ya mshahara wake hadi pauni laki moja kwa wiki.
Manchester City inaaminika kuwa iko tayari kutoa marupurupu mengine yatakayofikisha gharama yake hadi pauni milioni 40 japo wanalalamika kuwa Liverpool imeongeza maradufu thamani yake ikifahamika kuwa wenyewe hawakuwa hata wakimlipa pauni laki moja kwa juma.
Kwa habari , matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment