Dangote:Nitainunua Arsenal
Mfanyibiashara
tajiri zaidi barani Afrika kutoka Nigeria Aliko Dangote amesema kuwa
anapania kununua klabu ya Arsenal ya Uingereza.
Bilioneya huyo mmiliki wa kampuni ya kusafisha mafuta nchini Nigeria amesema fedha atakazopata kutoka kwa mauzo ya Mafuta na mijengona faida kutoka na uzalishaji wa mafuta zitamruhusu kununua klabu hiyo.
Tajiri huyo mwenye umri wa miaka 58 anasemekana anamiliki mali yenye thamani ya pauni bilioni 11.5.
Dangote amekuwa shabiki mkubwa wa Arsenal tangu miaka ya 80.
Bwanyenye mwenza kutoka Marekani Stan Kroenke anamiliki asilimia 66.64% ya kampuni inayomiliki klabu hiyo Arsenal Holdings plc.
Tajiri kutoka Urusi Alisher Usmanov anamiliki asilimia 29.11% huku hisa 62,217 zilizosalia zikimilikiwa na wachezaji wa zamani na mashabiki wa klabu hiyo.
Dangote ameorodheshwa katika nafasi ya 67 katika orodha ya matajiri zaidi duniani ya Forbes.
Awali Dangote alikuwa amependekeza kununua asilimia 15.9% ya hisa zilizopewa Kroenke kwa pauni milioni £123 ambao awali zilikuwa zinamilikiwa na Nina Bracewell-Smithin mnamo Aprili 2011 .
Dangote alijiondoa hata baada ya mazungumzo kuanza.
Dangote anasema kuwa Arsenal inahitaji umiliki mpya ilikuchochea mabadiliko na matokeo uwanjani.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment