Sunday, March 15, 2015

MAANDALIZI YA PAMBANO NA MAYWEATHER

Nyumba mpya ya Manny Pacquiao: familia yake itafikia kwa ajili ya pambano lake na Mayweather..

mansioBondia Manny Pacquiao ni dhahiri amejipanga vizuri kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuchukua ushindi dhidi ya mpinzani wake Floyrd Mayweather baada ya kununua jumba la kifahari alilokuwa anamiliki staa wa muziki Puff Dady, lililopo katika mji wa Bavery Hills.
Manny alifanya uamuzi huo baada ya kuridhishwa na nyumba hiyo yenye ukubwa wa futi 10,000 kwa kitita cha dola milioni 12.5 likiwa na kila kitu ndani yake.
Uamuzi huo umekuja ikiwa ni siku chache zimebakia kabla bondia huyo kupanda jukwaani katika pambano lake dhidi ya mpinzani wake Mayweather litakalofanyika May 2 Los Angeles, Marekani ambapo familia yake kutoka Ufilipino itafikia hapo.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia  www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment