HELKOPTA YADONDOKA,YAUA 4 DAR.
Sehemu ya mabaki ya Helikopta baada ya kuanguka Ajali
ambayo imedaiwa kuwa ni mali ya Maliasili na Utalii imegharimu maisha ya
marubani 3 wa Jeshi la Polisi Tanzania. Sp Kidai Kaluse, Insp.Simba
Must Simba, Pc. Josso Selestine, Na rubani mmoja Capt. Khalfan,Ajali
hiyo imetokea huko Kipunguni B Moshi Bar,Ukonga-Ilala jijini Dar es
Salaam. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la
ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sadick Meck Sadick akizungumza na Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali
hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne
Baadhi ya Wataalamu wakifanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya Helikopta.
Baadhi ya watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar,Ilala jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment