Wednesday, March 18, 2015

COLORADO PIA YAPATITISHA UHALALI WA MATUMIZI YA BANGI

Ninayo nyingine kuhusu mauzo ya Bangi kule walikohalalisha…

7004737-large
Unajua imekuwa hii ni ishu ambayo inakaa sana kwenye headlines, upande wa Bongo Sheria zimebanwa zaidi kuzuia matumizi ya dawa za kulevya, Marekani tukasikia story tofauti, wao kuna Majimbo ambayo yaliruhusu matumizi ya Bangi, uhalali huu umeingiza Bangi kuwa bidhaa halali kabisa kutumiwa na kuuzwa kama ilivyo bidhaa nyingine Majimbo kama ya Washington DC, Alaska.
Hii ya leo ni kwamba Jimbo la Colorado unaambiwa wamefanikiwa kukusanya kodi ambayo ni dola Mil. 15 (zaidi ya Bil. 27 Tshs).
Fungu hilo la kodi linapelekwa kujenga Shule mbalimbali kupitia mpango wa Jimbo hilo uliopewa jina la Building Excellent Schools Today (BEST)
Tangu kupitishwa utaratibu wa kuruhusu uuzaji wa bangi, unaambiwa maduka ya kuuza bidhaa hiyo rejareja mtaani kuanzia Jan. 1, 2014 mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya kodi ambayo ni dola Mil. 15 ambazo zinasaidia kuboresha mazingira ya Shule za Umma katika Jimbo hilo.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia muda wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment