Wednesday, March 18, 2015

MBUZI MWENYE VICHWA VIWILI AZALIWA KENYA

Uliipata hii ya maajabu ya mbuzi huyu kutoka Kenya?

DSC00655
Mbuzi mmoja katika Kijiji cha Kakanjuni Kenya amezaa mbuzi mwenye vichwa viwili vilivyoungana huku akiwa na midomo miwili, tukio hili limewashangaza wengi walioshuhudia huku wengine wakihisi kwamba mbuzi huyo ni mkosi.
Kahaso Ngumbao ambaye ndio anamfuga mbuzi huyo alitarajia mbuzi huyo angezaa mapacha kama kawaida yake lakini imekuwa tofauti, Wanakijiji wakitaka kumuua kwa madai kuwa ni mkosi kutokana na mila za jamii hiyo.
Kwa sasa mwenye mbuzi huyo kuamua kumpeleka mbuzi wake Makao makuu ya Kilimo kwa ajili ya kumhifadhi wanakijiji wasimuue.
MbuziVichwaViwili
Nilikuwa natafuta njia ya kupatia msaada wa huyu mnyama maana hawezi na nikiachiwa mimi huenda nikashindwa saa nyingine.. nikiachia watoto hawawezi kumlea vile ambavyo labda ningekuwa mimi mwenywe” — Kahaso Ngumbao
Afisa wa Kilimo, Wanyama na Samaki aliahidi kuwa Serikali ya kaunti hiyo itatafuta mahali mbadala na kumhifadhi mbuzi huyo.

No comments:

Post a Comment