M

BADO Mji wa Mafinga wilayani Mufindi haujakaa sawa kufuatia vifo vya watu 50 waliopoteza maisha kwa ajali ya kontena kudondokea Basi la Majinja lenye namba za usajili T 438 CED iliyotokea Machi 11, 2015,

Mtoto aliyenusurika kwenye ajali.
Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Changarawe mjini Mafinga ambapo kontena hilo lilikuwa kwenye lori la mizigo la Scania lenye namba za usajili T 689 APJ mali ya Kampuni ya Cipex lililokuwa likitokea Dar kwenda Mbeya huku basi hilo likitokea Mbeya kuelekea Dar.
KILICHOTOKEA BAADA YA AJALI
Kilichotokea baada ya ajali hiyo ni kuonekana kwa Mkono wa Mungu ambapo mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja mpaka miwili kunusurika katika ajali hiyo huku watu 50 wakipoteza maisha.
WAZAZI WA MTOTO
Akisimulia ilivyokuwa kwa wazazi wa mtoto huyo ambaye jina lake halijajulikana, mmoja wa abiria walionusurika, Aidan alisema kuwa, kabla ya kuanza safari jijini Mbeya, mtoto huyo alibebwa na mama yake akiwa ameongozana na abiria wengine.

Muonekano wa kontena lililosababisha ajali hiyo.
"Wazazi wa mtoto waliingia na kukaa siti ya tatu tu kutoka kwa dereva. Hakuna aliyehisi kwamba mbele ya safari kuna janga kubwa kama hili."Basi lilianza safari, kila abiria alikuwa akizungumza na mwenzake, wengine walikuwa wakiongea na simu. Wapo waliokuwa wakichati, nadhani ni wale wanaotumia WhatsApp. Kumbe bwana shetani alikuwa anatembea na sisi," alisema abiria huyo akiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mufindi.
No comments:
Post a Comment