Kumbe kuna Marais wanaoomba kupunguziwa muda wa kukaa madarakani..!

Stori
za viongozi wa Afrika kujiongezea muda wa kukaa madarakani ni kawaida
kusikika, lakini kusikia kwambe eti Rais wa nchi anaomba kupunguziwa
muda wa kukaa madarakani hii imekaa tofauti mtu wangu!
Rais wa Senegal, Macky Sall amependekeza
ipigwe kura ya maoni ambayo itafanya kuwe na mabadiliko ya Katiba
ambayo yatafanya muda wake wa kukaa madarakani upungue kutoka miaka saba
kwa muhula mmoja wa uongozi mpaka miaka mitano.
Rais
huyo amesema alichaguliwa kwa miaka saba lakini mwakani mwezi Mei
anapendekeza kufanyika kwa kura ya maamuzi ili kupunguza kwa muda wake
na kupisha wengine waendelee na nafasi hiyo.
Kama hili likitimia Rais Sall atakuwa
ametimiza moja ya ahadi aliyoahidi wakati wa Kampeni zake mwaka 2012
kwamba atafanya mabadiliko kwenye Katiba ili Rais akae madarakani kwa
miaka mitano badala ya saba.
No comments:
Post a Comment