Mashabiki wa Roma wakimbia uwanjani,wachezaji wafanya kazi ya ziada kuwaomba radhi.
Kiungo Danielle De Rossi akizungumza na mashabiki wa Roma…….
Mashabiki wa klabu ya As Roma ya nchini Italia walikimbia uwanjani baada ya kuishuhudia timu yao ikiwa nyuma kwa mabao 3:0 baada ya dakika 22 kwenye mchezo wa marudio raundi ya 16 bora ya kombe ya Europa dhidi ya ndugu zao Fiorentina.
Nahodha Francesco Totti ambaye jana hakucheza ilimbidi pia kwenda kuwatuliza mashabiki waliokuwa na hasira.
mara
baada ya Roma kufungwa bao la tatu kwenye dakika ya 22 mashabiki
waliamua kuondoka uwanjani kama picha inavyoonyesha hapo juu.
Uwanja ukiwa mtupu kipindi cha pili wakati mchezo ukiendelea……
No comments:
Post a Comment